Jumamosi, 23 Januari 2016

MFANO WA MATINI YA KIPRIGMATIKI: "FIMBO YANGU"

 JINA LA MWANACHUO: GABRIEL Sweetbert J

NAMBA YA USAJIRI: T/UDOM/2013/02815

KOZI:  BED-ECE                       

SWALI; Kutunga matini yenye maana ya kipragmatiki.

                                             



                                                             FIMBO YANGU
Nilinyoosha mkono, angalau kuishika fimbo ile lakini sikuweza! Kwani ilikuwa imedondoka katikati ya korongo. Korongo lile, lilikuwa refu kiasi cha mita tisa kwenda chini na upana wake ilikuwa kama mita sita hivi, katikati kulikuwa na maji machache yaliyotuama, yaliyoruhusu nyasi chache na miti mirefu kwa mifupi kusitawi. Ndani ya korongo lile walizunguka wanyama na wadudu wenye sumu kali ambao kila mara hawakuchoka kunimezea mate hasa pale, nilipojaribu kuitoa fimbo ile kwani ilikuwa karibu nidondoke ndani.
Taratibu nilijivuta kuelekea upande wa pili wa lile korongo, ambako niliona gogo kubwa lililokuwa limedondoshwa na Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa kiasi kama cha miaka minne iliyopita. Nilifanikiwa kushika gogo lile, na kutoka katika eneo lililojaa kila aina ya  hatari kwani ilikuwa karibu nidondoke korongoni, japokuwa sikufanikiwa kuigusa wala kuitoa fimbo ile, kwani ilikuwa imedondoka katikati ya korongo na kuzungukwa na ng’e  na  nyoka wenye sumu kali.
Moyoni nilijawa na simanzi kwani kushindwa kuitoa fimbo ile ambayo niliitafuta kwa kipindi cha muda mrefu , ilikuwa ni hatari kwa jamii yangu. Na isitoshe, “ilikuwa ni vigumu kuipata tena, na hata kama nitaipata itanichukua muda mrefu, kiasi kama cha miaka mitano hivi” nilijisemea. Nilijiuliza moyoni, hata kama  nitasubiri miaka mitano, nitaitoaje? Kwani, hata sehemu ya kujishikiza kuingia katika korongo itakuwa ngumu kuipata,  na pengine labda lile gogo litakuwa limeoza tayari, na hata kama lile gogo litakuwepo nani atanisaidia? ili hali wote wanaogopa kuitoa fimbo ile? Je vipi kuhusu Ng’e na Nyoka wale? Na kama nikishindwa, nani atafanikiwa kuitoa ili atawazwe kuwa kiongozi,  aiokoe jamii yetu?
Hayo yote, ni maswali yaliyomsumbua Mkombozi ndotoni, na ghafla aliinuka kutoka usingizini baada ya kusikia sauti ya jogoo akiwika. Aliinuka kwa unyonge kutoka usingizini, huku moyoni akihuzunika sana, kwani ndoto ile iligusa ukweli wa kile alichokuwa akiwaza kwa ajiri ya ukombozi wa jamii yao.
Mkombozi alinyanyuka kitandani taratibu kuelekea uwani, akimkumbuka marehemu babu yake  alivyo muhusia kabla hajaaga dunia  kuhusu Fimbo ile…

                            

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni