JINA LA MWANACHUO: GABRIEL Sweetbert J
NAMBA YA USAJIRI: T/UDOM/2013/02815
KOZI: BED-ECE
SWALI; Kutunga matini yenye maana ya kipragmatiki.
FIMBO
Nilinyoosha
mkono, angalau kuishika fimbo ile lakini sikuweza! Kwani ilikuwa imedondoka
katikati ya korongo. Korongo lile, lilikuwa refu kiasi cha mita tisa kwenda
chini na upana wake ilikuwa kama mita sita hivi, katikati kulikuwa na maji
machache yaliyotuama, yaliyoruhusu nyasi chache na miti mirefu kwa mifupi
kusitawi. Ndani ya korongo lile walizunguka wanyama na wadudu wenye sumu kali ambao
kila mara hawakuchoka kunimezea mate hasa pale, nilipojaribu kuitoa fimbo ile
kwani ilikuwa karibu nidondoke ndani.
Taratibu
nilijivuta kuelekea upande wa pili wa lile korongo, ambako niliona gogo kubwa
lililokuwa limedondoshwa na Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa kiasi kama
cha miaka minne iliyopita. Nilifanikiwa kushika gogo lile, na kutoka katika
eneo lililojaa kila aina ya hatari kwani
ilikuwa karibu nidondoke korongoni, japokuwa sikufanikiwa kuigusa wala kuitoa
fimbo ile, kwani ilikuwa imedondoka katikati ya korongo na kuzungukwa na ng’e na
nyoka wenye sumu kali.
Moyoni
nilijawa na simanzi kwani kushindwa kuitoa fimbo ile ambayo niliitafuta kwa
kipindi cha muda mrefu , ilikuwa ni hatari kwa jamii yangu. Na isitoshe, “ilikuwa
ni vigumu kuipata tena, na hata kama nitaipata itanichukua muda mrefu, kiasi
kama cha miaka mitano hivi” nilijisemea. Nilijiuliza moyoni, hata kama nitasubiri miaka mitano, nitaitoaje? Kwani,
hata sehemu ya kujishikiza kuingia katika korongo itakuwa ngumu kuipata, na pengine labda lile gogo litakuwa limeoza
tayari, na hata kama lile gogo litakuwepo nani atanisaidia? ili hali wote
wanaogopa kuitoa fimbo ile? Je vipi kuhusu Ng’e na Nyoka wale? Na kama nikishindwa,
nani atafanikiwa kuitoa ili atawazwe kuwa kiongozi, aiokoe jamii yetu?
Hayo
yote, ni maswali yaliyomsumbua Mkombozi ndotoni, na ghafla aliinuka kutoka
usingizini baada ya kusikia sauti ya jogoo akiwika. Aliinuka kwa unyonge kutoka
usingizini, huku moyoni akihuzunika sana, kwani ndoto ile iligusa ukweli wa
kile alichokuwa akiwaza kwa ajiri ya ukombozi wa jamii yao.
Mkombozi
alinyanyuka kitandani taratibu kuelekea uwani, akimkumbuka marehemu babu
yake alivyo muusia kabla hajaaga
dunia kuhusu Fimbo ile…
Maana
ya matini haya Kipragmatiki
Dhana
ya “Fimbo” inarejelea Uongozi katika jamii nyingi za kiafrika, na dhana ya
“Korongo” nimeitumia nikirejelea “Ukoloni” namna ambavyo ulijitokeza na
kutawanya tawala za kiafrika zilizoonesha upinzani. Kisa hiki kinaelezea namna
ambavyo Mkombozi anapoteza mamlaka ya kuongoza jamii yake, baada ya babu yake kuaga
dunia. Kwani, mamlaka yake yanachukuliwa mikononi mwa Wageni (Wakoloni) na
tunaona jinsi Mkombozi akiwa katika harakati za kurudisha mamlaka yake tena
kutoka mikononi mwa wakoloni hao, lakini kwa bahati mbaya hajafanikiwa...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni