Alhamisi, 16 Februari 2017

SHAIRI "NDOTO"

               "NDOTO "
Nikiwa kwa yangu ndoto, 
Nikawaona watoto, 
Kama wako kwenye moto, 
Ndani yake mna joto, 
Wakilia kitoto. 

Niliwaona vijana, 
Sitawataja kwa majina, 
Waliofanana watwana, 
Mbele ya hao mabwana, 
Waliodhani sio wana.

Niliwaona wazee,
Kwenye chumba kizee,
Wamefungiwa pekee,
Wakilia kizee,
Ati, hatuendelei mbelee.